Unganisha Kifaa cha sauti cha Bluetooth au onyesho pasi waya kwenye kompyuta yako
Unganisha kifaa cha sauti cha Bluetooth (Windows 10)
Ili kuunganisha vifaa vyako vya sauti, spika, au vipasa sauti kwenye kompyuta yako ya Windows 10, utahitaji kuunganisha kifaa kwanza.
Washa kifaa chako cha Bluetooth na ukifanye kigundulike.
Jinsi ya kukifanya kigundulike inategemea kabisa na kifaa. Angalia maelezo ya kifaa au tovuti ili kufahamu zaidi.
Kwenye mwambaa wa kazi, teua ikoni ya kituo cha kitendo, na uhakikishe Bluetooth imewashwa.
Kwenye kituo cha vitendo, teua Unganisha, kicha chagua kifaa chako.
Fuata maagizo yoyote ya ziada. Vinginevyo, umekamilisha.
Maonyesho pasi waya ya MIracast
Unganisha kompyuta yako bila waya kwenye Televisheni, projekta, au aina nyingine ya onyesho la nje linaloauni Miracast.
Washa Televisheni au projekta yako. Kama unatumia Miracast dongle au adapta, hakikisha imechomekwa kwenye onyesho.
Hakikisha Wi-Fi imezimwa kwenye kompyuta yako.
Kwenye mwambaa wa kazi, teua ikoni ya kituo cha kitendo > Unganisha > chagua onyesho lako.
Fuata maagizo yoyote ya ziada kwenye skrini. Vinginevyo, umekamilisha.
Onyesho pasiwaya la WiGig
Unganisha kompyuta yako bila waya kwenye monita, projekta, au aina nyingine ya onyesho la nje ambalo limeunganishwa kwenye egesho la WiGig.
Washa Televisheni au projekta.
Washa egesho lako la WiGig na uhakikishe limeunganishwa kwenye onyesho.
Hakikisha kompyuta yako inaauni WiGig na imewashwa. Iwapo kompyuta yako inaauni WiGig, utaona kidhibiti cha WiGig kwenye Mipangilio > Mtandao na Intaneti > Modi ya ndege.