Je, Windows Hello ni nini?
Windows 10
Windows Hello ni ya kibinafsi zaidi, njia salama zaidi ya kufikia papo hapo kwenye vifaa vyako vya Windows 10 kwa kutumia utambuzi alama ya kidole, sura, au mboni yako.
Kompyuta nyingi zilizo na visomaji vya alama ya vidole ziko tayari kutumia Windows Hello sasa, na vingi zaidi ambavyo vinaweza kutambua sura na mboni yako vinakuja hivi karibuni. Iwapo una kifaa tangamanifu cha Windows Hello, hapa kuna jinsi ya kukisanidi:
Windows 10 Mobile
Windows Hello ni njia ya binafsi zaidi ya kuingia kwenyeWindows 10. Hutambua macho yako ili kuthibitisha utambulisho wako, ambao humaanisha unapata usalama wa gredi ya biashara bila kucharaza kwenye nywila.
Windows Hello huweka vipi faragha ya maelezo yangu?
Baadhi ya simu za Lumia zinazoendesha Windows 10 ziko tayari kutumia Windows Hello sasa, na vifaa vingi ambavyo vina utambuzi wa mboni vinakuja hivi karibuni.
Washa Anza, Telezesha kwenye orodha ya programu Zote, na kisha uteue Mipangilio > Akaunti > Chaguo za kuingia.
Pindi umesanidi, utaweza kufungua simu yako kwa mtazamo.