Jinsi ya kutumia programu ya Ving’ora na Saa
Ondosha au sinzia ving’ora
Ving’ora vitatoa sauti hata kama programu imefungwa, sauti imenyamazishwa, kompyuta yako imefungwa, au (katika baadhi ya kompyuta za mkononi au kompyuta kibao ambazo zina InstantGo), kwenye modi Kusinzia.
Lakini havitafanya kazi wakati kompyuta yako inasinzia au imezimwa. Hakikisha umechomeka kompyuta yako kwenye nishati ya AC ili kuizuia kutokana na kusinzia.
Ili kusinzia au kuondosha king’ora:
Kwenye taarifa ibukizi, teua Ondosha ili kuizima, au Sinzia ili kuifanya itoe sauti tena baada ya muda mfupi.
Iwapo taarifa hufunga kabla uifikie, teua ikoni ya kituo cha kitendo kwenye kona ya chini kulia ili kuiona kwenye orodha na uiteue kutoka hapo.
Iwapo skrini yako imefungwa, taarifa ya kingo’ra huonekana upande wa juu wa skrini ya kufunga, na unaweza kuizima kutoka hapo.
Ni nini kipya
Vingo’ra na programu ya Saa huchanganya saa ya kingo’ra na saa za ulimwengu, kipima muda, na kipima wakati. Hapa kuna mambo machache unayoweza kufanya kwa programu hii:
Sikiliza, sinzia, na uondoshe ving’ora hata wakati skrini imefungwa au sauti imenyamazishwa
Chagua sauti tofauti au muziki wako binafsi kwa king’ora
Linganisha saa kote ulimwenguni
Saa za dunia
Hapa kuna jinsi ya kuongeza eneo na kulinganisha saa kote ulimwenguni:
Kwenye programu ya Ving’ora na Saa, teua Saa ya Dunia, na kisha Mpya + upande wa chini.
Ingiza herufi chache za kwanza za eneo unalotaka, na kisha lichague kwenye orodha kunjuzi. Iwapo huoni unalotaka, ingiza eneo jingine ambalo liko kwenye ukanda sawa wa saa.
Teua Linganisha saa (saa 2 katika upande wa chini), na kisha sogeza kitelezeshi ili kuchagua muda mpya wa kulinganisha. Teua eneo kwenye ramani ili kubadilisha eneo ambalo kitelezeshi kinarejelea.
Ili kutoka kwenye modi ya Linganisha Saa, teua kitufe cha Nyuma , au bonyeza Esc.