rekebisha miunganisho kwenye vifaa vya sauti vya bluetooth na mionekano ya pasi waya kwenye windows 10 mobile

Weka miunganisho kwenye vifaa vya sauti vya Bluetooth na maonyesho ya pasiwaya

Sauti ya Bluetooth

Iwapo kubonyeza kitufe cha Unganishakwenye kituo cha kitendo hakupati kifaa chako cha sauti kilichowezeshwa kwa Bluetooth, jaribu hii:
Hakikisha kifaa chako cha Windows kinauni Bluetooth na kimewashwa.

Utaona kitufe cha Bluetooth kwenye kituo cha kitendo.
Hakikisha kuwa kifaa cha sauti kilichowezeshwa kwa Bluetooth kimewashwa na kinatambulika. Jinsi ya kufanya hii hutofautiana kwa vifaa, kwa hivyo angalia maelezo ambayo yalikuja na kifaa chako au nenda kwenye tovuti ya mtengenezaji.
Iwapo unatafuta vifaa vilivyowezeshwa kwa Bluetooth mbali na sauti, nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio wa Bluetooth. Nenda kwenye Mipangilio, teua Vifaa, teua Bluetooth, teua kifaa, teua Ondoa kifaa, na kisha ujaribu kuunganisha tena.

Vifaa vya Miracast

Iwapo kubonyeza kitufe cha Unganishakwenye kituo cha kitendo hakupati kifaa chako, jaribu hii:
Hakikisha kifaa chako cha Windows kinaauni Miracast kwa kukagua maelezo yaliyokuja nacho au kwa kuenda kwenye tovuti ya mtengenezaji.
Hakikisha Wi-Fi imewashwa.
Hakikisha onyesho unalotaka kuonyesha linaauni Miracast na kuwa limewashwa. Iwapo hakiauni, utahitaji adapta ya Miracast (wakati mwingine inaitwa “dongle”) ambayo huchomekwa kwenye kituo cha HDMI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *